Mfumo wa mauzo na hesabu kwa maduka ya Tanzania.

Duka lako,
kiganjani mwako.

Andika mauzo, stoo na madeni. Jua faida yako halisi kila siku — hata bila mtandao.

Ipate kwenye Google Play

Siku 14 bure, bila kadi ya benki

DUKA LA AMANI

Risiti #1042 · 14:20

2 × Sukari 1kg6,000
1 × Mafuta 1L8,500
3 × Sabuni3,600
JUMLATZS 18,100

Asante, karibu tena!

Ichapishe kwa printa ya thermal ya 80mm au 58mm, au itume kwa WhatsApp.

  • Inafanya kazi bila mtandao
  • Printa ya Bluetooth na A4
  • Kila mfanyakazi na namba yake ya siri
  • Kiswahili na Kiingereza

Jinsi ya kuanza

Anza kwa hatua tatu

  1. Jisajili kwa namba yako

    Weka namba ya simu na jina la duka lako. Hakuna fomu ndefu wala kadi ya benki.

  2. Weka bidhaa zako

    Ziweke moja moja, au ingiza orodha nzima kutoka Excel — kila bidhaa na bei yake ya kununua na ya kuuza.

  3. Anza kuuza

    Gusa bidhaa, chagua njia ya malipo, mpe mteja risiti. Programu inakuhesabia faida yenyewe.

Kazi zake

Kila unachohitaji dukani, mahali pamoja

Uza haraka

Gusa bidhaa au skani barcode, chagua njia ya malipo, chapisha risiti. Ni sekunde chache tu.

Jua kilichopo stoo

Kipi kimebaki, kipi kinakaribia kuisha, na kipi hakitoki kabisa.

Fuatilia madeni

Nani unamdai, nani anakudai, kiasi gani na tangu lini.

Ona faida halisi

Si mauzo tu — ni faida baada ya kutoa gharama za bidhaa na matumizi yote.

Mtandao ukikatika, biashara inaendelea.

Kila kitu kinahifadhiwa kwenye simu yako kwanza. Mtandao ukirudi, kinatumwa chenyewe — hakuna mauzo yanayopotea.

  1. Imehifadhiwa kwenye simuMtandao umekatika — mauzo yanaendelea
  2. ImetumwaMtandao umerudi — kila simu imeipata

Aina za maduka

Imetengenezwa kwa ajili ya duka kama lako

Kila aina ya duka inakuja na makundi yake ya bidhaa tayari — huhitaji kuyaandika mwenyewe.

  • Duka la jumla / rejareja

    Vyakula · Vinywaji · Sabuni

  • Duka la dawa

    Vidonge · Sindano · Vifaa

  • Duka la vifaa vya ujenzi

    Saruji · Mabati · Rangi

  • Baa / Mgahawa

    Vinywaji · Chakula

Bei

Bei iko wazi, hakuna cha kushtukiza

Kifurushi ni kimoja tu. Hakuna cha bei ya juu chenye vitu vya ziada.

Miezi 6

60,000

TZS kwa tawi moja

Takriban 10,000 kwa mwezi

Mwaka mmoja

100,000

TZS kwa tawi moja

Takriban 8,300 kwa mwezi

Unaokoa zaidi

Kuanzia tawi la pili, kila tawi ni nusu bei. Lipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas au Airtel Money ndani ya programu.

Kwa bei zote, unapata

  • Mauzo, stoo, madeni na matumizi
  • Faida ya kila siku, kila bidhaa na kila mfanyakazi
  • Wafanyakazi kadiri unavyohitaji, kila mmoja na ruhusa zake
  • Risiti kwa karatasi ya 80mm, 58mm na A4
  • Inafanya kazi bila mtandao
  • Msaada kwa simu na WhatsApp

Maswali

Maswali yanayoulizwa sana

Siku 14 zikiisha, inakuwaje?

Duka lako halifungwi. Utaendelea kuona kila kitu ulichoweka — mauzo, stoo, ripoti — lakini hutaweza kuandika mauzo mapya mpaka ulipe. Taarifa zako zinabaki kuwa mali yako.

Kweli inafanya kazi bila mtandao?

Ndiyo. Kila kitu kinahifadhiwa kwenye simu yako kwanza, na mtandao ukirudi kinatumwa chenyewe. Unaweza kuuza siku nzima bila bando na hupotezi chochote.

Muuzaji wangu ataona faida na ripoti zangu?

Hapana, isipokuwa ukitaka. Muuzaji anaona tu kile anachohitaji ili kuuza. Ripoti, bei ya kununua na mipangilio ni kwa ajili ya mmiliki na meneja tu.

Nahitaji printa gani?

Printa yoyote ya thermal ya 80mm au 58mm — zile zinazouzwa Kariakoo. Kama huna printa, tuma risiti kwa WhatsApp au ihifadhi kwa ukubwa wa A4.

Nikiwa na matawi mawili au zaidi?

Kila tawi la ziada ni nusu bei — 50,000 TZS kwa mwaka. Unabadilisha tawi ndani ya programu, na ripoti zinaonyesha kila tawi peke yake au yote kwa pamoja.

Nahitaji kompyuta?

Hapana. Simu inatosha. Profit Lite inafanya kazi kwenye simu, tablet au kompyuta — kupitia programu ya Android au kupitia tovuti.

Simu yangu ikipotea au ikiharibika?

Ingia kwenye simu nyingine kwa namba yako. Kila kitu kilichokwisha kutumwa mtandaoni kinarudi — bidhaa, mauzo, madeni na wafanyakazi. Ndiyo maana ni vizuri simu ipate mtandao angalau mara moja kwa siku.

Naweza kuuza kwa mkopo?

Ndiyo. Uza kwa mkopo, na ukurasa wa Madeni unaonyesha kila mteja anadaiwa kiasi gani. Akilipa kidogo kidogo, pokea malipo yake na deni litapungua lenyewe.

Inasoma barcode?

Ndiyo. Kwenye ukurasa wa Mauzo, skani barcode ya bidhaa kwa kamera ya simu. Pia kila risiti inaonyesha namba yake kama barcode chini kabisa.

Nina bidhaa nyingi — lazima niziandike moja moja?

Hapana. Ingiza orodha nzima kutoka faili la CSV — Excel inaweza kuhifadhi orodha yako kama CSV.

MafunzoJinsi ya kutumia Profit, hatua kwa hatua

Anza leo. Una siku 14 za kujaribu.

Unahitaji namba ya simu tu. Ukiona haikufai, taarifa zako zinabaki kuwa mali yako.

Ipate kwenye Google Play

Inapakia…